Habari
ya siku kadhaa zilizopita ndugu msomaji , natumai u mzima wa afya, ila kama ni
kinyume na hapo ukajikuta upo katika hari ambayo kuna mapungufu ya kiafya basi
Mungu akupe heri mapema ili ufanikiwe kuludi katika shughuli zako ili kuyajenga
maisha yako.
Kama
ilivyo ada leo nakuja tena kwako ili tupeane mawazo ambayo kama kwa pamoja tukiayazingatia na
kuyaweka katika matendo basi mafanikio ni lazima.
Leo
nnapenda kuongelea kuhusu ”MACHAGUZI”,
huenda sio neno geni machoni pako lakini limetokana na neno uchaguzi
ikiwa na maana ya hari ya kuchagua kitu au vitu kutoka katika vitu vingine.
Kila
binadamu ameumbwa na hali hii ya uchaguzi ndani yake ndio maana wote hatuwezi
kufanya kitu kimoja ndani ya dunia hii, ukiitazam dunia jinsi inavyoendeshwa
utagundua ni mkusanyiko wa vipaji
mbalimbali hapa naongelea wahandisi, wahasibu, wanasiasa, wansayansi, mama
ntilie, makondakta, madreva, madaktari ,waalimu na wengineo maana siwezi
nikawataja wote. Ila tambua kuwa Kila
unaemuona yupo katika nafasi flani hata kama ni ndogo kiasi gani au ni kubwa
sana amini kwamba ni uchaguzi wake menyewe kuwa katika hali hii.
Katika
dunia hii unaweza ukawa mtu wa namna yoyote ile unayotaka, ila kama ukiamua
kuwa hivyo, yaani namaanisha uwe na maamuzi sahihi na usiwe mtu wa kutanga
tanga na kila kinachopita mbele yako. Yaani labda ulitamani kuwa mwalimu lakini
kwa kuwa umesikia uhandisi unalipa ukaamua kuacha na ualimu ukangia huko, na
baada ya muda ukisikia udreva unamaslahi zaidi basi ukabadili maamuzi na
kuingia katika udreva , kamwe tambua kwamba kwa hali hii kamwe hautafanikiwa
katika maisha yako bali utaishia kupoteza
muda wako bure.
Yeyote
unaemuona amefanikiwa katika jambo lolote lile iwe ni biashara au chochote kile
tambua kuwa aliwekeza muda wa kutosha katika kujifunza kufanya jambo hilo na
alikosea mara kadhaa na akakubali kujifunza kutokana na makosa yake na ndio
maana unaona anafanya kitu bora kama hicho. Leo nnaomba nikupe baadhi ya mbinu
kuwa n a uchaguzi bora. Na mbinu hizo ni kama hizi zifuatazo:-
- Weka malengo halisi na
yanayotimizika: siku zote weka malengo kulingana
na uwezo wako, kulingana na kipato chako. Usije ukania mambo makubwa sana
kuliko vile ulivyo na ukumbuke kuayapanga katika muda, yaani kila lengo
unalopanga ulipe muda sahihi n a uhakikishe umelishughulikia ndani ya muda
ulioupanga. Hii itakusaidie zaidi kusonga mbele.
- Fanya Jambo Moja Kwa Wakati
Mmoja: Imeshawahi kukutokea jua
linazama na upo njiani kuelekea nyumbani na unahisi umechoka kupita kiasi
na huwezi kukumbuka kitu ulichofanikiwa kukifanya na kukimaliza katika
siku unayoimalizia? Jibu lako laweza kuwa ndio. Kinachotokea katika
mazingira ya namna hiyo ni kwamba ulijaribu kufanya kila kitu kwa wakati
mmoja.Pamoja na ukweli kwamba sote tungependa sana kutimiza mambo mengi
kwa wakati mmoja ukweli hatari zaidi ni kwamba akili zetu hazijaumbwa
hivyo. Unapoanza kufanya jambo moja na ghafla ukashika lingine,akili yako
nayo hugeukia upande huo, hivyo hata katika maisha yako yote chagua kitu
kimoja na ukifanye kwa ufanisi. Tofauti na hapo utajikuta kila kitu
unakifanya kwa kubahatisha.
Uwezo wetu unakuwa maradufu
tunapofanya kitu kimoja kwa wakati mmoja badala ya kujaribu kurukia mambo kumi
kwa wakati mmoja. Tunao msemo usemao “mtaka yote hukosa yote”. Ni kweli kabisa.
Malengo tunayojiwekea ni ya aina nyingi. Kuna ya muda mfupi na muda mrefu. Yote
yanahitaji kutulia kwa akili zetu. Jitahidi kukamilisha jambo moja kabla ya
kurukia lingine. Utagundua kwamba kwa kufanya hivyo unakamilisha mambo mengi
zaidi. Unashauriwa kugawa siku yako katika vipindi vya muda. Jiambie kwamba
katika saa hii nitakuwa nafanya hesabu ya mzigo, au nitakuwa shambani. Katika
saa inayofuatia, nitakuwa kwenye mkutano. Utatimiza mengi zaidi. Mbinu nzuri
pia ni kuziweka katika muda fulani kazi au majukumu yanayoshabihiana. Kwa mfano
kama unafanya kazi za ubunifu, weka mambo yanayoendana na ubunifu kwa wakati
mmoja tofauti na masuala ya utawala.
Kimsingi kuna njia nne za kukamilisha
jambo au jukumu. Aidha unalimaliza, unaachana nalo,unampa mtu mwingine au
unalipa wakati tofauti au kwa kifupi unaliahirisha. Unapojiwekea malengo, ni
muhimu pia kuangalia uwezo wako katika kukamilisha malengo hayo. Endapo wewe tu
ndio mwenye uwezo na rasilimali za kukamilisha lengo au malengo fulani,basi
fanya hivyo. Lakini endapo unahisi, kwa sababu moja au nyingine ikiwemo uwezo
na rasilimali, huwezi kukamilisha jambo,basi usisite kugawa jukumu hilo kwa mtu
mwingine.
Kugawa jukumu kwa mtu mwingine ni njia nzuri na mbadala ya
kukamilisha lengo. Lakini pia usisite kuahirisha kufanya jambo fulani katika
wakati fulani hususani kama halina umuhimu zaidi ya lingine. Na usijisikie
vibaya.Hujashindwa. Umelisogeza mbele au kulipa wakati mwingine. Na mwisho kama
unahisi lengo fulani halina umuhimu tena, basi achana nalo.
Fata mpango kazi wako. Watu mara nyingi wanaweza kutengeneza mpango
kazi na ratiba vizuuri. Ila sasaaa ngoja kwenye kuifata ndipo kuna utata.
Ukitaka kuacha kupoteza mda wako basi fata ratiba ya kazi zako uliyoitengeza
mwenyewe. Baati nzuri unakua umeipanga mwenyewe. Yaani Fuata Ratiba
uliyoitengeneza maana hiyo ndio muongozo wa kazi zako za kila siku. Hii iko
hivi ratiba yako ulipanga saa sita unaenda mahara kuchukua mzigo na kuupeleka
huko unakotakiwa kwenda na una uhakika kabisa utaenda, ila cjui kwa nini
unaacha kwenda huko mahara hiyo saa sita unasema kwanza uende sokoni kununua
kitu kingine.
siku zote kumbuka kuwa uchaguzi sahihi
ndio mafanikio sahihi.....na kama unataka mafanikio halisi jifunze kufany
auchaguzi bora!
tukutane
tena katika mada zijazo.....
