Kabla hatujaenda mbali ni vema kwanza tukajiuliza nini maana halisi ya maisha.....
Maana ya maisha ni nini? Nawezaje kupata utimilifu au kutimiza malengo na kutosheka maishani mwangu? Je, nitafanikiwa kuwa na uwezo wa kutimiza jambo la kudumu? Watu wengi hatujaacha kufikiria juu ya maana ya maisha ni nini. Wengi wetu hufikiri sana hasa kuhusu kule tulikotoka na kuvunjika moyo, na mara baada ya hapo hujiona kutofaa na kuwa hawawezi kabisa!
Tunapoyatazama maisha ya siku zilizopita tunapata makundi mengi sana ambayo nitayataja kwa kifupi:
1) Kundi la kwanza ni kundi la wale waliopoteza malengo.
Hapa mtu alikuwa na ndoto kubwa za mafanikio ambazo alikuwa amejiwekea, na
kuamini kwamba zitakuwa sawa, lakini kwa kadri maisha yanavyokwenda anakuja kugunduaa
kwamba hawezi tena, na hii ilitokea baada ya kuwa amepata kazi ambayo hakuitegemea, au
alikutana na mtu ambae alimdhania kuwa ndie na kumbe sie, lakini pia kujikuta mahala
ambapo hakutarajia kujikuta.
2) Kundi la pili ni la wale waliokata tamaa....
Hawa ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wameona kwamba ni bora waseme
"inatosha sasa, juhudi zote nilizowekeza katika kukabiliana na maisha lakini bado sijapata
mafanikio kama wengine, basi labda ndivyo Mungu alivyoniandikia" na mara baada ya kauli hii
ndani ya mtu huyu hujisikia kuridhika na vile alivyojifariji na mara baada ya hapo huacha kila
kitu kijiendeshe chenyewe pasipo yeye kujihusisha sana,
3) Kundi la tatu ni wale wanaoyaona maisha kama mipango kutoka mahala flani
watu wa namna hii siku zote huamini kwamba maisha ni vile ulivyopangiwa na Mungu, na
ukimuuliza wewe Mungu alikupangia kitu gani ....unakuja kugundua kuwa hana la maana
ispokuwa anatumia lugha hii kama njia ya kujihami, ili jamii isimuone kuwa hajishughulishi
Mara baada ya kuyatazama makundi haya kwa uchache hebu tuludi kwenye swali letu, "maisha ni nini"
Maisha ni jumla ya shughuli zote azifanyazo kiumbe (kwenye mada hii ni binadamu) toka kutungwa mimba hadi pale moyo (kiungo
chenye kazi ya kusukuma damu mwilini sehemu zote za mwili na hivyo
kuurutubisha mwili kwani damu ndiyo njia kuu ya usafirishaji mwilini) utakapokoma kufanya kazi yake.
Katika maisha ya kila binadamu kuna shughuli zinazofanana kwa viumbe
wote na kuna shughuli zinazotofautiana toka binadamu mmoja hadi
mwingine. Kwa kawaidaa shughuli zote za kimaumbile za binadamu hufanana.
Shughuli hizo ni pamoja na zile zifanyikazo ndani ya mwili wa binadamu;
na zile zinazofanyika nje ya mwili wake, ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo zaidi ya kumi na tano inayoshirikiana, Baadhi ya
mifumo iliyo mwilini mwa binadamu ni pamoja na mfumo wa usafirishaji
ambapo moyo na mishipa mwilini husafirisha damu na vyakula sehemu zote
za mwili. Upumuaji ni mfumo unaotumia idara za pua, mapafu na kadhalika
kuwezesha upumuaji wa mwili. Utoaji taka mwilini huhusisha idara kadhaa
na hata mifumo mingine kufanya kazi hiyo...Na nje ya mwili wa binadamu pia kuna mfumo ambao amepewa uwezo kutoka ndani yake kuja nje ili kuweza kuyatawala mazingira yake. Hari hii amepewa kila bianadmu na ndio maana unaona kila binadamu amejawa na hari ya kutoridhika na vile alivyo leo, bali hutamani siku zote kuwa bora Zaidi kuliko kiumbe mwengine yeyote!
Pamoja na shughuli zinazofanana kwa binadamu wote kuna mahitaji ya lazima ambayo ni muhimu kwa kila binadamu bila kuzingatia nafasi zao kijamii, kiuchumi na kadhalika. Chakula, hewa safi, na hifadhi ya namna Fulani ( mazingira bora ya kuishi) ni kati ya mahitaji ya lazima kwa binadamu wote.
Ili aweze kuishi vyema na mwili wake ufanye kazi, binadamu analazimika kula - lazima apate chakula katika kipindi fulani ili mwili wake uendelee kupata mahitaji na virutubisho vinavyouwezesha mwili kuendelea kuishi, hali kadhalika hewa safi. Ili mwili uendelee na kazi zake lazima upate hewa safi. Binadamu wote huhitaji hifadhi ya namna fulani; toka kwenye mavazi hadi nyumba ya kujihifadhi, ni ubora tu ndiyo hutofautiana toka mmoja hadi mwingine.
Hivyo ni jukumu la kila binadamu kuhakikisha kuwa ili aweze kufanikiwa katika kila jambo nililolieleza hapo juu ni jukumu lake kupambana kwa kila hali ili kuweza kupata maisha bora Zaidi!
na ili kuanikiwa katika hilo ni vema ukajiunga na mtandao wa AMSHA MAISHA ambao huu utakuwa ukukikupatia Makala mbalimbali zitakazokusaidia wewe kujikwamua kutoka katika hari mbaya uionayo leo kwenda hari nzuri.
No comments:
Post a Comment