Wednesday, June 10, 2015

HAPA NDIPO PENYE UFANISI





 
Habari ya siku kadhaa zilizopita ndugu msomaji , natumai u mzima wa afya, ila kama ni kinyume na hapo ukajikuta upo katika hari ambayo kuna mapungufu ya kiafya basi Mungu akupe heri mapema ili ufanikiwe kuludi katika shughuli zako ili kuyajenga maisha yako.
Kama ilivyo ada leo nakuja tena kwako ili tupeane mawazo ambayo kama  kwa pamoja tukiayazingatia na kuyaweka katika matendo basi mafanikio ni lazima.
Leo nnapenda kuongelea kuhusu ”MACHAGUZI”,  huenda sio neno geni machoni pako lakini limetokana na neno uchaguzi ikiwa na maana ya hari ya kuchagua kitu au vitu kutoka katika vitu vingine.
Kila binadamu ameumbwa na hali hii ya uchaguzi ndani yake ndio maana wote hatuwezi kufanya kitu kimoja ndani ya dunia hii, ukiitazam dunia jinsi inavyoendeshwa utagundua ni mkusanyiko wa  vipaji mbalimbali hapa naongelea wahandisi, wahasibu, wanasiasa, wansayansi, mama ntilie, makondakta, madreva, madaktari ,waalimu na wengineo maana siwezi nikawataja wote.  Ila tambua kuwa Kila unaemuona yupo katika nafasi flani hata kama ni ndogo kiasi gani au ni kubwa sana amini kwamba ni uchaguzi wake menyewe kuwa katika hali hii.
Katika dunia hii unaweza ukawa mtu wa namna yoyote ile unayotaka, ila kama ukiamua kuwa hivyo, yaani namaanisha uwe na maamuzi sahihi na usiwe mtu wa kutanga tanga na kila kinachopita mbele yako. Yaani labda ulitamani kuwa mwalimu lakini kwa kuwa umesikia uhandisi unalipa ukaamua kuacha na ualimu ukangia huko, na baada ya muda ukisikia udreva unamaslahi zaidi basi ukabadili maamuzi na kuingia katika udreva , kamwe tambua kwamba kwa hali hii kamwe hautafanikiwa katika maisha yako bali utaishia kupoteza  muda wako bure.
Yeyote unaemuona amefanikiwa katika jambo lolote lile iwe ni biashara au chochote kile tambua kuwa aliwekeza muda wa kutosha katika kujifunza kufanya jambo hilo na alikosea mara kadhaa na akakubali kujifunza kutokana na makosa yake na ndio maana unaona anafanya kitu bora kama hicho. Leo nnaomba nikupe baadhi ya mbinu kuwa n a uchaguzi bora. Na mbinu hizo ni kama hizi zifuatazo:-
  • Weka malengo halisi na yanayotimizika: siku zote weka malengo kulingana na uwezo wako, kulingana na kipato chako. Usije ukania mambo makubwa sana kuliko vile ulivyo na ukumbuke kuayapanga katika muda, yaani kila lengo unalopanga ulipe muda sahihi n a uhakikishe umelishughulikia ndani ya muda ulioupanga. Hii itakusaidie zaidi kusonga mbele.
  • Fanya Jambo Moja Kwa Wakati Mmoja: Imeshawahi kukutokea jua linazama na upo njiani kuelekea nyumbani na unahisi umechoka kupita kiasi na huwezi kukumbuka kitu ulichofanikiwa kukifanya na kukimaliza katika siku unayoimalizia? Jibu lako laweza kuwa ndio. Kinachotokea katika mazingira ya namna hiyo ni kwamba ulijaribu kufanya kila kitu kwa wakati mmoja.Pamoja na ukweli kwamba sote tungependa sana kutimiza mambo mengi kwa wakati mmoja ukweli hatari zaidi ni kwamba akili zetu hazijaumbwa hivyo. Unapoanza kufanya jambo moja na ghafla ukashika lingine,akili yako nayo hugeukia upande huo, hivyo hata katika maisha yako yote chagua kitu kimoja na ukifanye kwa ufanisi. Tofauti na hapo utajikuta kila kitu unakifanya kwa kubahatisha.
Uwezo wetu unakuwa maradufu tunapofanya kitu kimoja kwa wakati mmoja badala ya kujaribu kurukia mambo kumi kwa wakati mmoja. Tunao msemo usemao “mtaka yote hukosa yote”. Ni kweli kabisa. Malengo tunayojiwekea ni ya aina nyingi. Kuna ya muda mfupi na muda mrefu. Yote yanahitaji kutulia kwa akili zetu. Jitahidi kukamilisha jambo moja kabla ya kurukia lingine. Utagundua kwamba kwa kufanya hivyo unakamilisha mambo mengi zaidi. Unashauriwa kugawa siku yako katika vipindi vya muda. Jiambie kwamba katika saa hii nitakuwa nafanya hesabu ya mzigo, au nitakuwa shambani. Katika saa inayofuatia, nitakuwa kwenye mkutano. Utatimiza mengi zaidi. Mbinu nzuri pia ni kuziweka katika muda fulani kazi au majukumu yanayoshabihiana. Kwa mfano kama unafanya kazi za ubunifu, weka mambo yanayoendana na ubunifu kwa wakati mmoja tofauti na masuala ya utawala.
Kimsingi kuna njia nne za kukamilisha jambo au jukumu. Aidha unalimaliza, unaachana nalo,unampa mtu mwingine au unalipa wakati tofauti au kwa kifupi unaliahirisha. Unapojiwekea malengo, ni muhimu pia kuangalia uwezo wako katika kukamilisha malengo hayo. Endapo wewe tu ndio mwenye uwezo na rasilimali za kukamilisha lengo au malengo fulani,basi fanya hivyo. Lakini endapo unahisi, kwa sababu moja au nyingine ikiwemo uwezo na rasilimali, huwezi kukamilisha jambo,basi usisite kugawa jukumu hilo kwa mtu mwingine.
 Kugawa jukumu kwa mtu mwingine ni njia nzuri na mbadala ya kukamilisha lengo. Lakini pia usisite kuahirisha kufanya jambo fulani katika wakati fulani hususani kama halina umuhimu zaidi ya lingine. Na usijisikie vibaya.Hujashindwa. Umelisogeza mbele au kulipa wakati mwingine. Na mwisho kama unahisi lengo fulani halina umuhimu tena, basi achana nalo. 
 Fata mpango kazi wako. Watu mara nyingi wanaweza kutengeneza mpango kazi na ratiba vizuuri. Ila sasaaa ngoja kwenye kuifata ndipo kuna utata. Ukitaka kuacha kupoteza mda wako basi fata ratiba ya kazi zako uliyoitengeza mwenyewe. Baati nzuri unakua umeipanga mwenyewe. Yaani Fuata Ratiba uliyoitengeneza maana hiyo ndio muongozo wa kazi zako za kila siku. Hii iko hivi ratiba yako ulipanga saa sita unaenda mahara kuchukua mzigo na kuupeleka huko unakotakiwa kwenda na una uhakika kabisa utaenda, ila cjui kwa nini unaacha kwenda huko mahara hiyo saa sita unasema kwanza uende sokoni kununua kitu kingine.
siku zote kumbuka kuwa uchaguzi sahihi ndio mafanikio sahihi.....na kama unataka mafanikio halisi jifunze kufany auchaguzi bora!
 tukutane tena katika mada zijazo.....


 

 

Friday, June 5, 2015

"Maana ya maisha ni nini?"

Karibu mpenzi msomaji wa blog ya amsha maisha, hapa ni sehemu ambayo tunaweza kubadilishana mawazo ya aina mbalimbali ili kuweza kupata maana halisi ya maisha yetu katika nyanja mbalimbali kama vile nyanja za kiuchumi, kiroho, kijamii na mambo kadha wa kadha!
 Kabla hatujaenda mbali ni vema kwanza tukajiuliza nini maana halisi ya maisha.....

Maana ya maisha ni nini? Nawezaje kupata utimilifu au kutimiza malengo na kutosheka maishani mwangu? Je, nitafanikiwa kuwa na uwezo wa kutimiza jambo la kudumu? Watu wengi hatujaacha kufikiria juu ya maana ya maisha ni nini. Wengi wetu hufikiri sana hasa kuhusu kule tulikotoka na kuvunjika moyo, na mara baada ya hapo hujiona kutofaa na kuwa hawawezi kabisa!

Tunapoyatazama maisha ya siku zilizopita tunapata makundi mengi sana ambayo nitayataja kwa kifupi:
   1) Kundi la kwanza ni kundi la wale waliopoteza malengo.
          Hapa mtu alikuwa na ndoto kubwa za mafanikio ambazo alikuwa amejiwekea, na
          kuamini  kwamba zitakuwa sawa, lakini kwa kadri maisha yanavyokwenda anakuja kugunduaa
          kwamba hawezi tena, na hii ilitokea baada ya kuwa amepata kazi ambayo hakuitegemea, au
          alikutana na mtu ambae alimdhania kuwa ndie na kumbe sie, lakini pia kujikuta mahala
          ambapo hakutarajia kujikuta.
2) Kundi la pili ni la wale waliokata tamaa....
         Hawa ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wameona kwamba ni bora waseme
         "inatosha sasa, juhudi zote nilizowekeza katika kukabiliana na maisha lakini bado sijapata
         mafanikio kama wengine, basi labda ndivyo Mungu alivyoniandikia" na mara baada ya kauli hii
         ndani ya mtu huyu hujisikia kuridhika na vile alivyojifariji na mara baada ya hapo huacha kila
         kitu kijiendeshe chenyewe pasipo yeye kujihusisha sana,
3) Kundi la tatu ni wale wanaoyaona maisha kama mipango kutoka mahala flani
        watu wa namna hii siku zote huamini kwamba maisha ni vile ulivyopangiwa na Mungu, na
        ukimuuliza wewe Mungu alikupangia kitu gani ....unakuja kugundua kuwa hana la maana
        ispokuwa anatumia lugha hii kama njia ya kujihami, ili jamii isimuone kuwa hajishughulishi

Mara baada ya kuyatazama makundi haya kwa uchache hebu tuludi kwenye swali letu, "maisha ni nini"
Maisha ni jumla ya shughuli zote azifanyazo kiumbe (kwenye mada hii ni binadamu) toka kutungwa mimba hadi pale moyo (kiungo chenye kazi ya kusukuma damu mwilini sehemu zote za mwili na hivyo kuurutubisha mwili kwani damu ndiyo njia kuu ya usafirishaji mwilini) utakapokoma kufanya kazi yake.
Katika maisha ya kila binadamu kuna shughuli zinazofanana kwa viumbe wote na kuna shughuli zinazotofautiana toka binadamu mmoja hadi mwingine. Kwa kawaidaa shughuli zote za kimaumbile za binadamu hufanana. Shughuli hizo ni pamoja na zile zifanyikazo ndani ya mwili wa binadamu; na zile zinazofanyika nje ya mwili wake, ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo zaidi ya kumi na tano inayoshirikiana, Baadhi ya mifumo iliyo mwilini mwa binadamu ni pamoja na mfumo wa usafirishaji ambapo moyo na mishipa mwilini husafirisha damu na vyakula sehemu zote za mwili. Upumuaji ni mfumo unaotumia idara za pua, mapafu na kadhalika kuwezesha upumuaji wa mwili. Utoaji taka mwilini huhusisha idara kadhaa na hata mifumo mingine kufanya kazi hiyo...

 Na nje ya mwili wa binadamu pia kuna mfumo ambao amepewa uwezo kutoka ndani yake kuja nje ili kuweza kuyatawala mazingira yake. Hari hii amepewa kila bianadmu na ndio maana unaona kila binadamu amejawa na  hari ya kutoridhika na vile alivyo leo, bali hutamani siku zote kuwa bora Zaidi kuliko kiumbe mwengine yeyote!

Pamoja na shughuli zinazofanana kwa binadamu wote kuna mahitaji ya lazima ambayo ni muhimu kwa kila binadamu bila kuzingatia nafasi zao kijamii, kiuchumi na kadhalika. Chakula, hewa safi, na hifadhi ya namna Fulani ( mazingira bora ya kuishi)  ni kati ya mahitaji ya lazima kwa binadamu wote.
Ili aweze kuishi vyema na mwili wake ufanye kazi, binadamu analazimika kula - lazima apate chakula katika kipindi fulani ili mwili wake uendelee kupata mahitaji na virutubisho vinavyouwezesha mwili kuendelea kuishi, hali kadhalika  hewa safi. Ili mwili uendelee na kazi zake lazima upate hewa safi. Binadamu wote huhitaji hifadhi ya namna fulani; toka kwenye mavazi hadi nyumba ya kujihifadhi, ni ubora tu ndiyo hutofautiana toka mmoja hadi mwingine.
Hivyo ni jukumu la kila binadamu kuhakikisha kuwa ili aweze kufanikiwa katika kila jambo nililolieleza hapo juu ni jukumu lake kupambana kwa kila hali ili kuweza kupata maisha bora Zaidi!
 na ili kuanikiwa katika hilo ni vema ukajiunga na mtandao wa AMSHA MAISHA ambao huu utakuwa ukukikupatia Makala mbalimbali zitakazokusaidia wewe kujikwamua kutoka katika hari mbaya uionayo  leo kwenda hari nzuri.